Klabu ya APR FC kutoka Rwanda imeingia katika kinyang’anyiro cha kumuwania mshambuliaji kutoka Asec Mimosa Ecua Acua Celestine ambaye amefunga jumla ya magoli 15 ndani ya msimu huu akiwa na klabu hiyo ya Asec mimosas ya nchini Ivory coast.
Vilabu vya Simba pamoja na Yanga sc za nchini ni miongoni mwa vilabu vilivyoonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo kuelekea msimu ujao.
Hata hivyo kitendo cha Apr Fc kuingilia dili hilo hakiwazuii majayanti wa soka Afrika Mashariki na kati kumsajili staa huyo kutokana na kuwa na bajeti kubwa ya fedha za usajili.
Mshambuliaji huyo amegeuka lulu msimu huu wa ligi kuu nchini humo akifunga jumla ya mabao 13 kwenye ligi kuu sambamba na kutoa pasi za mabao 10 mpaka sasa.
Kutokana na takwimu hizo ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya nchini humu ambapo katika misimu mitatu iliyopita waliotwaa tuzo hizo Stephan Aziz Ki,Pacome Zouzoua na Jean Charles Ahoua wote wamesajiliwa hapa nchini.