Site icon Sports Leo

Klabu ya Simba sc inaangalia namna ya kumsajili mlinzi wa kulia wa klabu ya Azam Fc, Lusajo Mwaikenda ambapo mpaka sasa wawakilishi wa beki huyo  wamefanya mazungumzo na Simba sc kuona namna ya kumpata mlinzi huyo.

Mpaka sasa bado kuna ugumu wa kumpata nyota huyo kwasababu klabu yake ya Azam Fc bado inahitaji hudama yake ingawa mchezaji mwenyewe anatamani kuondoka klabuni hapo ili akapate changamoto sehemu nyingine.

Bado mazungumzo yanaendalea kati ya wasimamizi wa mchezaji na uongozi wa Azam Fc ili kumuachia nyota huyo kwenda sehemu mpya na kama uongozi wa klabu yake ya sasa utaridhia basi ofa itatumwa klabuni hapo.

Lusajo anatamani kuondoka katika mazingira ya amani kutokana na klabu hiyo kuwa ndio iliyomlea na kuibua kipaji chake na sasa imempa unahodha huku akiwa na uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.

Exit mobile version