Home Soka APR Yaitoa Azam Fc Caf

APR Yaitoa Azam Fc Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imekubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika hatua ya awali uliofanyika katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali na kufuta ndoto za klabu hiyo za kushiriki hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Azam Fc ilihitaji ushindi ama sare ya aina yeyote ili kufuzu hatua ya pili ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika lakini ndoto hiyo ilipotea ilipokubali bao la kwanza dakika ya 45 likifungwa na Jean Bosco Ruboneka.

Kipindi cha pili Azam Fc inayonolewa na makocha Bruno Ferry na Yousouph Dabo ilianza vizuri huku ikipaki basi kwa asilimia kadhaa lakini mambo yalibadilika dakika ya 62 ilipokubali goli la Gilbert Byiringilo na kufuta kabisa ndoto za klabu hiyo.

banner

Azam Fc ilijitahidi kutafuta walau bao moja ili kurejesha umakini lakini ilijikuta ikikoswa koswa yenyewe kufungwa kutokana na kushindwa kurejea kwa wakati pindi wanapopoteza mpira.

Apr sasa baada ya kufuzu hatua ya pili itakua na kazi ngumu ya kupambana na Pyramids Fc ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Sasa mabosi wa Azam Fc hawana cha kupoteza na wanarejea nchini kufanya tathmini juu ya ubora wa benchi la ufundi la klabu hiyo huku makocha wakuu wakiwekwa kitimoto kuhusu hatma yao klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited