Beki wa Manchester United Ashley Young ameigomea timu yake kufanya mazoezi na kutimkia ndani ya kikosi cha Inter Milan.
Mchezaji huyo amekubali kujiunga na Inter Milani inayoshiriki serie A akitokea kwenye timu inayoshiriki ligi kuu England kutokana na kutokufurahishwa na maisha yake ndani ya Manchester United.
Mabosi wa Inter Milan wameweka mezani pauni milioni 15 ili kupata saini ya mchezaji huyo na hivi karibuni baada ya kuchukuliwa vipimo atajiunga nao katika kikosi hicho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ashley Young ameigomea Manchester United kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na anahitaji kuondoka kwenye usajili wa mwezi Januari licha ya mkataba wake kumeguka mwishoni mwa msimu huu.