Home Makala Azam Fc Mbabe Dhidi ya Singida FG

Azam Fc Mbabe Dhidi ya Singida FG

by Sports Leo
0 comments

Azam Fc imeibuka kidedea na kufanikiwa kubeba alama zote tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Fountain Gate Fc baada ya kuifunga timu hiyo kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Azam Fc ilianza kupata bao la mapema dakika ya 10 lililofunga na Cheikh Sidibe kwa shuti kali la faulo lililomshinda kipa Beno Kakolanya ambapo baada ya bao hilo Azam Fc waliukamata mchezo huku Singida FG wakijitahidi kusawazisha bila mafanikio huku Prince Dube akikosa nafasi kadhaa za wazi.

Kipindi cha pili Marouf Tchakei alifunga bao la kusawazisha kwa shuti kali nje ya 18 lililojaa wavuni moja kwa moja huku Singida FG nao wakirudi mchezoni lakini kukosa umakini kwa Bruno Gomez,Duke Abuya na Elvis Rupia.

banner

Azam FC walilazimika kuzitumia vyema dakika tano za nyogeza ambapo Idd Nado alifunga bao kwa kichwa baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa timu ya Singida FG ambapo bao hilo lilidumu mpaka mpira ulipomalizika.

Sasa Azam Fc nao wanafikisha alama tisa katika nafasi ya tatu ya msimamo huku Yanga sc wakiwa kileleni na Simba sc katika nafasi ya pili huku Singida FG wakiangukia katika nafasi ya 12 wakiwa na alama mbili katika michezo mitatu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited