Klabu ya Azam Fc imeshindwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Mashujaa Fc uliofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Azam Fc ilishindwa kupata bao lolote licha ya kocha Rachid Taoussi kuamua kuanza na mshambuliaji Jhonier Blanco ambaye hakumtumia michezo miwili iliyopita ambapo ilimlazimu kumtoa mapema kipindi cha pili na kumuingiza Nassoro Saiduni ambaye naye hakua na wakati mzuri huku shuti lake kali la dakika ya mwisho ya mchezo almanusura liwape bao Azam Fc baada ya kugonga mwamba wa juu wa goli.

Mashujaa Fc walikosa bahati mara kadhaa katika mchezo huo baada ya kukosa nafasi za wazi kupitia kwa mshambuliaji wake Crispin Ngushi ambapo kipa Mohamed Mustapha aliibuka shujaa kwa kuokoa michomo hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Azam Fc sasa imecheza michezo sita ya ligi kuu ikiambulia alama tisa pekee ikiwa nafasi ya tano ya msimamo huku Mashujaa Fc ikiwa nafasi ya sita ikicheza michezo mitano ikiwa na alama tisa katika nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.
