Home Soka Azam Fc Yajitoa Kagame Cup

Azam Fc Yajitoa Kagame Cup

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Azam Fc ya jijini Dar es salaam imetangaza kujitoa katika michuano ya soka ya Kagame Cup inayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Visiwani Zanzibar kuanzia Julai 6 mwaka huu katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.

Akitangaza uamuzi huo Meneja wa Idara ya habari ya klabu hiyo Zakaria Thabit alisema kuwa timu hiyo haitashiriki michuano hiyo kutokana na ratiba ya michuano hiyo kuingiliana na ratiba ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/2025.

“Azam Fc haitoshiriki michuano hiyo ya Kagame kutokana na timu kuwa kwenye mapumziko mpaka tarehe 4 julai ndipo wachezaji watarejea kuanza pre seasons,Tarehe hizo zitakuwa ngumu kwetu kutokana na wachezaji  wote wanatakiwa kukaa press session zaidi ya wiki sita na hii kwa mujibu wa kitalaamu  timu iwe tayari kwa mashindano ”amesema Meneja habari Azam FC  Zakaria Thabit maarufu kama Zaka Zakazi.

banner

Awali michuano hiyo ilipangwa kufanyika nchini Sudan lakini kutokana na hali ya kisiasa kutotengemaa basi iliwalazimu Cecafa kuihamishia michuano hiyo Zanzabar huku Sudan wakipewa nafasi ya kuingiza timu nne kama mwenyeji ambapo timu za El Merreikh, Al Hilal, Hai El Wadi zitashiriki huku Tanzania ikiingiza timu za Simba sc,Yanga sc,Azam Fc na Coastal union na Rwanda ikiingiza timu ya APR na Vital O kutoka nchi ya Burundi itashiriki.

Timu nyingine ni Gor Mahia (Kenya), SC Villa (Uganda), JKU SC (Zanzibar), El Merreikh FC-Bentiu (Sudan Kusini), Nyasa Big Bullets (Malawi), TP Mazembe (DR Congo) na Red Arrows (Zambia) ambazo zitaungana na timu alikwa kuunda timu 16 zitakazoshiriki michuano hiyo inayodahminiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited