Home Soka Azam Fc Yalambishwa Asali Tabora

Azam Fc Yalambishwa Asali Tabora

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc uliofanyika katika uwanja wa Al Hassan Mwinyi mkoani humo.

Makocha wote wawili waliingia na vikosi vyao kamili ambapo Rachid Taoussi aliwaanzisha Mohammed Mustapha,Lusajo Mwaikenda ambaye alikua nahodha wa kikosi hicho wakiwa sambamba na mastaa wengine wa kikosi hicho wakiwemo Gibril Sillah,Feisal Salum huku Heritier Makambo na Morris Chukwu wakiongoza safu ya ushambuliaji ya Tabora United.

Heritier Makambo alikua mwiba mkali kwa Azam Fc akionyesha kiwango mahiri kabisa ambapo dakika ya 38 ya mchezo aliunganisha kwa kichwa krosi iliyoipa Tabora United bao la uongozi.

banner

Kipindi cha pili Azam Fc walijipanga vyema lakini uimara wa Tabora United waliocheza mchezo huo kwa umoja na nguvu kubwa uliwazuia kupata bao.

Dakika ya 68 Makambo tena aliwazidi maarifa mabeki wa Azam Fc na kupata bao la pili akimchungulia kipa Mohamed Mustapha na kuufanya uwanja kujaa kwa shange na nderemo kubwa.

Azam Fc waliongeza kasi ya kushambulia na kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Yoro Diaby lakini haliwakuzuia Tabora United kuchukua alama tatu.

Azam Fc sasa imesalia na alama zake 30 kileleni mwa msimamo ikicheza michezo 14 huku Tabora United ikifikisha alama 24 katika michezo yake 14 ya ligi kuu katika nafasi ya tano ya msimamo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited