Klabu ya Azam Fc imempa mkataba wa miaka mitatu kocha Ahamid Moallin kuwa kocha wa kikosi hicho baada ya kushikiria nafasi hiyo kama kocha wa muda akirithi mikoba ya George Lwandamina aliyetimuliwa mwaka jana.
Moallin awali aliajiriwa kama mkurugenzi wa ufundi klabuni hapo akihusika hasa na kukuza soka la vijana lakini matokeo mabaya ya kikosi cha wakubwa chini ya kocha George Lwandamina ”Chicken Man” hali iliyompeleka kutimuliwa klabuni hapo na nafasi hiyo kuangukia kwa Moallin kama kaimu kocha mkuu.
Matokeo mazuri pamoja na kiwango kizuri cha uchezaji wa timu kwa ujumla kumewashawishi mabosi wa klabu hiyo kumpa mkataba kocha huyo huku ushindi dhidi ya Prisons wa 4-0 ugenini ukiwashtua wadau wengi wa soka nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Azam FC ni klabu kubwa, na nililiona hili siku ya kwanza tu nilipofika hapa, nina amini katika klabu hii, nina amini katika uwezo wa klabu hii, klabu hii ina nafasi ya kufanya makubwa,” Alisema Abdihamid Moallin.