Home Makala Azam Fc Yasajili Mashine Mpya

Azam Fc Yasajili Mashine Mpya

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Azam FC imekamilisha usajili wa beki raia wa Ivory Coast Zouzou Landry akitokea katika klabu ya Afad Djekanou ya nchini humo.

Zouzou mwenye umri wa miaka 23, anamudu kucheza beki ya kati (LCB) na beki ya kushoto (LB), amesaini mkataba wa miaka minne kuwepo kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2028.

Kocha Rachid Taoussi amepitisha usajili huo kuja kuchukua nafasi ya Yanick Bangala ambaye ametemwa klabuni hapo baada ya kiwango chake kutowaridhisha benchi la ufundi la klabu hiyo.

banner

Zouzoua ataungana na mabeki Yoro Diaby pamoja na Yeisson Mandoza kuunda ukuta wa hatari kwa timu hiyo inayoshika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania.

Hivi karibuni mabosi wa Azam Fc wamehamia Afrika Magharibi hasa nchi za Ivory coast na Mali kusajili mastaa wa maana klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited