Sports Leo

Azam Fc Yatua Kwa Yona Amos

Klabu ya Azam Fc Yatua Kwa Yona Amos kuihitaji saini ya mlinda lango wa klabu ya Pamba Jiji yenye makao yake jijini mwanza ili kuongeza machaguo kuelekea msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya Kimataifa.

Tayari mabosi wa klabu hiyo wamefahamishwa juu ya mkataba wa mwaka mmoja wa mchezaji huyo uliosalia na Pamba jiji na sasa wamerejea kuufanyia kazi ili kuangalia namna gani watampata mlinda lango huyo anayeongoza ndani ya ligi kuu ya Nbc akiwa na takwimu ya kuokoa hatari mara nyingi zaidi langoni.

Msimu huu kipa huyo ameokoa hatari langoni mara 69
katika michezo 28 Ya ligi kuu huku akicheza mechi 11 bila kuruhusu bao langoni mwake na akitwaa tuzo ya mchezaji bora mara 3 msimu huu.

Yona aliibukia katika klabu ya Tanzania Prisons msimu wa 2023-2024 ambapo alisajiliwa na Pamba jiji Fc msimu huu ulioisha ambapo kote huko amekua na kiwango bora sana.

Exit mobile version