Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki amefanikiwa kutwaa tuzo tatu katika tuzo za ligi kuu nchini zilizotolewa na Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kwa wanasoka waliofanya vizuri msimu wa 2023/2024 zilizofanyika katika ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa soka.
Katika usiku huo Aziz ambaye aliingia katika kinyang’anyiro akiwania takribani tuzo tatu za mchezaji bora wa msimu,Kiungo bora na mfungaji bora ambayo alikua na uhakika nayo baada ya kufunga idadi kubwa ya mabao katika msimu uliomalizika wa ligi kuu ya Nbc akifunga mabao 21.
Aziz Ki alitwaa tuzo zote hizo tatu alizokua anagombania na kumshinda mshindani wake wa karibu Feisal Salum ambaye hakupata tuzo katika ligi kuu japo alifanikiwa kuingia katika kikosi bora cha msimu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezaji huyo pamoja na kushinda tuzo hizo binafsi aliisaidia klabu yake ya Yanga sc kumaliza bingwa katika ligi kuu na michuano ya kombe la shirikisho la Crdb katika fainali zilizofanyika visiwani Zanzibar.
