Kiungo wa Yanga SC Stephane Aziz Ki na mlinzi wa Simba SC na Valentino Nouma wameachwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichoitwa jana na kocha Brama Traore kwaajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026

Burkina Faso itakuwa nyumbani Machi 16 2025 kucheza mchezo wake wa 5 wa hatua ya makundi dhidi ya Djibouti kabla ya kusafiri kuwafuata Guinea Bissau tarehe 23 Machi 2025
Ikumbukwe kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwepo katika kikosi kilichocheza mechi za mwanzoni za michuano hiyo akicheza michezo mitatu na kutoa pasi moja ya goli
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
The Stallions wanashika nafasi ya 3 katika kundi A ikivuna alama 5 katika michezo minne iliyocheza, nyuma ya Guinea Bissau yenye alama 6 na Misri mwenye alama 10 anayeongoza msimamo wa kundi hilo.
