Home Makala B/Mkapa Yafungwa Tena

B/Mkapa Yafungwa Tena

by Sports Leo
0 comments

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo imetangaza kuufunga uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ili kuufanyia ukarabati mwingine kuanzia leo April 10 2025.

Uamuzi huo umekuja baada ya jana kufanyika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba Sc dhidi ya Al Masry ya nchini Misri ambapo Simba sc ilifanikiwa kufuzu nusu fainali ikipata ushindi wa matuta 4-1 baada ya sare ya 2-2 katika michezo miwili.

banner

Uwanja huo jana ulitumika kukiwa na Mvua kubwa iliyonyesha uwanjani hapo dakika chache kabla ya mchezo huo kuanza na kusababisha uwanja kujaa matope ambapo pia nyasi ziliharibika kutokana na maji na matope hayo.

Hata hivyo uwanja huo hutumika kwa ruhusa maalumu kutokana na kuwa kwenye ukarabati mkubwa ili kuurudisha kwenye ubora wake.

Uwanja wa Benjamin Mkapa ni moja ya viwanja bora kabisa nchini na Afrika mashariki na kati huku ukichukua watu elfu sitini waliokaa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited