Site icon Sports Leo

Bakayoko Kubaki Napoli

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Stamford Bridge huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiendelea kuitamanisha klabu ya Napoli ambapo yupo kwa mkopo.

Kiungo huyo alisajiliwa na Chelsea akitokea Monaco ya nchini Ufaransa ambako aling’ara lakini kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha Chelsea alijikuta anakaa benchi mpaka klabu hiyo ilipomtoa kwa mkopo.

Exit mobile version