Beki wa kati wa Simba Sc Hussein Kazi anamaliza mkataba wake na wekundu wa msimbazi mwishoni mwa msimu huu ambapo anahusishwa kuondoka katika klabu hiyo baada ya msimu huu kumalizika na hakuna mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo ya Kariakoo mpaka sasa.
Taarifa za awali inatajwa kuwa klabu ya Namungo Fc inamuhitaji Hussein Kazi na dirisha lililopita la uhamisho Namungo Fc walimuhitaji Hussein Kazi kwa mkopo lakini Simba SC hawakuwa na nia hiyo ya kumuachia mchezaji huyo.
Simba sc ilimsajili Kazi kutoka Geita Gold Fc kwa mkataba wa miaka miwili ambapo sasa beki huyo amepoteza nafasi kikosini humo baada ya kusababisha penati katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita dhidi ya Yanga sc akimuangusha Stephan Aziz Ki ambaye alifunga penati hiyo na Simba sc kupoteza kwa mabao 2-1.
Katika eneo la beki wa kati ya Simba Sc Abdulrazak Hamza na Chamou Karabou wamekua wakianza siku za karibuni baada ya kuumia kwa Che Malone Fondoh huku Kazi mara nyingi akianzia benchi ama kukaa jukwaani.