Home Makala Brazil Waichapa Serbia

Brazil Waichapa Serbia

by Sports Leo
0 comments

Timu ya taifa ya Brazil imefanikiwa kuibuka na alama tatu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Serbia katika mchezo uliofanyika usiku na kuhudhuriwa na mashabiki wengi waliokua na shangwe la kutosha hasa baada ya vijana wa Samba kupata mabao mawili.

Ikianza na mastaa kama Neymar,Richarlison,Rafinha huku nyuma ikiwa na Thiago Silva na Marquinhos Brazil ilimiliki mchezo karibia dakika zote tisini ambapo dakika ya 62 shuti la Vinicius Jr lilipanguliwa na kipa Vanja Milinkovic-Savic na kumkuta mfungaji Richarlison aliyemaliza kwa shuti na kuipa uongozi timu hiyo.

Akipokea pasi ya Rodrygo dakika ya 70 Richarlison alionyesha kwanini anastahili kuanza dhidi ya Gabriel Jesus wa Arsenal baada ya kufunga kwa kiki ya kubinuka na kusababisha shangwe katika uwanja wa Lusail Stadium nchini Qatar akifunga magoli tisa katika michezo saba ya taifa lake huku pia akifunga katika mchezo wake wa kwanza wa kombe la dunia.

banner

Katika mchezo huo Neymar alifanikiwa kubanwa na Serbia huku akichezewa faulo tisa na kuweka rekodi ya kuchezewa faulo nyingi katika kombe la dunia la mwaka huu ambapo pia mkongwe Thiago Silva alifanikiwa kuonyesha kiwango kikubwa licha ya kuwa na umri wa miaka 38 na siku 63.

Ushindi huo Brazil sasa imefikisha alama tatu na kukaa juu ya msimamo wa kundi G wakiizidi Switzerland ilyoifunga Cameroon 1-0 ambapo watakutana siku ya jumatatu ijayo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited