Wachezaji wa klabu ya Simba sc Rally Bwallya na Mzamiru Yassin wamerejea klabuni hapo kutoka katika matatizo ya kifamilia na majeraha waliyokua nayo na kuwafanya yawaondoe kikosini kwa kipindi kifupi kilichopita.
Klabu hiyo iliwakosa mastaa hao ambao walikua na matatizo mbalimbali ikiwemo Bwallya aliyekua na msiba wa mwanafamilia wa karibu na kumlazimu kwenda nchini Zambia kushughulikia matatizo hayo huku Mzamiru Yassin akikumbwa na majeraha kiasi pamoja na matatizo ya kifamilia.
Simba sc iliwakosa mastaa katika mchezo dhidi ya Rs Berkane ambao uliisha kwa Simba sc kufungwa mabao 2-0 na kushushwa katika msimamo wa ligi ya kombe la shirikisho barani Afrika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.