Kiungo Carlos Stenio Fernandes maarufu kama Carlinhos Saa rasmi ataikosa Derby ya Kariakoo baada ya kutakiwa kukaa nje ya Uwanja kwa Wiki mbili.
Daktari wa timu ya Yanga , Shecky Mngazija amesema vipimo vya MRI , vimeonyesha kwamba nyota huyo amepata majeraha kwenye msuli wa paja alipotolewa nje kwenye mchezo wa kufuzu hatua ya robo fainali kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons.
“Kutokana na jeraha hili matibabu yatachukua takriban wiki mbili , hivyo hatakuwa sehemu ya programu ya benchi la ufundi katika kipindi hiki cha matibabu , ” amesema Dkt . Mngazija.
Amesema pamoja na Carlinhos beki Yassin Mustapha pia atakuwa nje kwa wiki mbili kutokana na kumia msuli wa paja pia.
Japo Yassin ameonekana kuchukua muda mrefu lakini anaendelea vyema , vipimo vinaonyesha maendeleo makubwa ya uponaji hivyo baada ya wiki mbili tuntarajie kurejea”
Amesema Dk mgazija.