Home Soka Che Malone Aomba Radhi Simba Sc

Che Malone Aomba Radhi Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Beki wa klabu ya Simba Sc  Che Malone Fondoh ameomba msamaha kutokana na makosa ambayo ameyafanya  kwenye mechi dhidi ya Bravo’s do Maquis yaliopelekea Bravo’s kupata goli 1.

Shukrani kwa bao la kusawazisha la Lionel Ateba na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 1-1 na kuifanya Simba sc kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kombe la Shirikisho  nchini.

Hata hivyo si mara ya kwanza kwa Che Malone kufanya makosa ya aina hiyo ikikumbukwa kuwa katika mchezo dhidi ya CS Sfaxien alifanya kosa kama hilo na kupelekea kuigharimu timu yake.

banner

“Natamani kuomba msamaha kwa familia nzima ya Simba Sc kwa makosa yangu kuigharimu timu na ninaahidi kufanya kazi kwa bidii ili kufanya vizuri siku zijazo”,Ulisomeka Ujumbe huo kupitia mitandao ya kijamii wa mchezaji huyo.

Che Malone Fondoh amekua na makosa ya mara kwa mara yanayopelekea mashabiki wa klabu hiyo kuanza kukosa imani na kiwango chake klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited