Beki wa klabu ya Simba Sc Che Malone Fondoh ameomba msamaha kutokana na makosa ambayo ameyafanya kwenye mechi dhidi ya Bravo’s do Maquis yaliopelekea Bravo’s kupata goli 1.
Shukrani kwa bao la kusawazisha la Lionel Ateba na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 1-1 na kuifanya Simba sc kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kombe la Shirikisho nchini.
Hata hivyo si mara ya kwanza kwa Che Malone kufanya makosa ya aina hiyo ikikumbukwa kuwa katika mchezo dhidi ya CS Sfaxien alifanya kosa kama hilo na kupelekea kuigharimu timu yake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Che Malone Fondoh amekua na makosa ya mara kwa mara yanayopelekea mashabiki wa klabu hiyo kuanza kukosa imani na kiwango chake klabuni hapo.