Home Makala Che Malone,Camara Hatihati Simba Sc

Che Malone,Camara Hatihati Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Wachezaji Che Malone Fondoh pamoja na kipa Moussa Camara wana hatihati ya kucheza mchezo ujao dhidi ya Coastal Union kutokana na kusumbuliwa na majeraha waliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Azam Fc.

Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 2-2 ulishuhudia Che Malone akiumia na kutolewa mapema kipindi cha kwanza huku kipa Camara akigongana na Zidane Sereri dakika za mwisho wa mchezo huo wakati akijitahidi kuokoa hatari langoni mwake.

banner

Kutokana na majeraha hayo mastaa hao walikosekana katika mazoezi ya jana jioni ambapo ilishuhudiwa makipa Ally Salim na Hussein Abel sambamba na kipa Alexander Erasto kutoka timu ya vijana wakishiriki mazoezi hayo.

Simba sc inakabiriwa na mchezo mgumu siku ya Jumamosi machi 1 dhidi Coastal Union ugenini katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Simba Sc endapo itawakosa mastaa hao haitatetereka kutokana na kujaa kwa wachezaji wa maana kikosini akiwemo kipa Ally Salim na beki Chamou Karabou ambao wataziba mapengo hayo.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Simba sc ina alama 51 katika nafasi ya pili ya msimamo ikicheza michezo 20 ya ligi kuu mpaka sasa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited