Home Makala Coastal Union Yakabidhiwa Basi Jipya

Coastal Union Yakabidhiwa Basi Jipya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Coastal Union yenye makazi yake jijini Tanga imekabidhiwa basi jipya aina ya Youtong na benki ya biashara ya Nbc nchini kwa ajili ya kurahisisha safari zake katika michuano mbalimbali inayoshiriki nchini ikiwemo ligi kuu ya Nbc.

Basi hilo jipya limekabidhiwa mapema Machi 22 jijini Tanga na Mkurugenzi wa biashara wa benki ya Nbc Elvis Nduguru na kupokelewa na mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batrida Buriani.

banner

Kutolewa kwa basi ni sehemu ya mkopo maalumu ambao benki ya Nbc imekua ikitoa kwa vilabu vya ligi kuu nchini ambapo mpaka sasa takribani shilingi bilioni 1.2 zimetumika mpaka sasa.

Coastal union inaungana na vilabu vya Kmc Fc,Namungo Fc,Singida Black Stars ambazo zote zimenufaika na mkopo huo.

Mbali na mkuu wa Wilaya ya Lushoto pia Mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union Hassan Muhsin pamoja na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo sambamba na wachezaji walihudhuria hafla hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited