Home Soka Dodoma Jiji Yamgeukia Makambo

Dodoma Jiji Yamgeukia Makambo

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Dodoma Jiji Fc sasa imeingilia dili la mshambuliaji wa zamani Yanga, Heritier Makambo kutoka Al Murooj SC ya Libya ambaye alikua katika mchakato wa kurejea nchini kujiunga na klabu ya Tabora United inayoshiriki ligi kuu ya Nbc msimu ujao.

Awali Mkongomani huyo aliyewahi kuzichezea DC Motema Pembe, FC Lupopo zote za DR Congo na Horoya AC ya Guinea, ilielezwa angejiunga na Tabora United na tayari mazungumzo yalifikia pazuri lakini  kwa sasa mambo yamebadilika baada ya Dodoma kumtaka.

Makambo binafsi yuko tayari kujiunga na klabu zote hizo mbili huku itakayoweka maslahi mazuri zaidi ndiyo itapewa kipaumbele ambapo mpaka sasa ofa ya Dodoma Jiji inaonekana kuwa kubwa na inamshawishi zaidi staa huyo maarufu kwa kushangilia kwa staili ya “kuwajaza”.

banner

Makambo aliondoka nchini mwaka 2019 baada ya kuuzwa na Yanga sc kwenda kujiunga na Horoya Fc ya nchini Guinnea ambapo baada ya miaka miwili alirejea Yanga sc ambapo mambo hayakuwa mazuri na kuondoka kujiunga na Al murooj ya nchini Libya.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited