Site icon Sports Leo

Domayo Nje kwa Majeraha

Kiungo wa Azam FC, Frank Domayo, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mguu.

Domayo aliumia mguu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe uliochezwa hivi karibuni na kumalizika kwa sare ya 1-1 uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex


Akizungumza na Sportsleobongo, Afisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, amesema: “Domayo atakaa nje kwa muda wa mwezi mmoja kwa majeraha ya mguu aliyoyapata kwenye mchezo wetu na TP Mazembe.”

Huyu ni kati ya wachezaji mahiri kwenye kikosi cha Azam kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiitumikia timu hiyo uwanjani tangu ajiunge nayo mwaka 2014 akitokea kunako klabu ya Yanga sc.
.

Exit mobile version