Site icon Sports Leo

Ericksen Azinduka

Mchezaji wa klabu ya  Inter Milan na Timu ya Taifa ya Denmark, Christian Eriksen Jumamosi iliyopita alianguka uwanjani na kupoteza fahamu kutokana na tatizo la moyo (cardiac arrest) katika dakika ya 42 ya mechi ya Euro 2020 Denmark dhidi ya  Finland.

Taarifa mpya kuhusu Eriksen  ni kwamba bado yupo hospitali akipatiwa matibabu lakini anaendelea vizuri na ametumia ukurasa wake wa instagram kuwashukuru wote waliomuombea wakati alipopata matatizo.

“Asante sana kwa salamu zenu nzuri na ujumbe kutoka ulimwenguni kote, ina maana kubwa sana kwangu na familia yangu niko sawa na bado ninahitajika kupitia vipimo hospitalini lakini ninajihisi sawa na sasa nitawashangilia vijana kwenye Timu ya Denmark katika mechi zijazo” ——— Christian Eriksen.

Ericksen ni miongoni mwa Wachezaji wa soka waliowahi kuitembelea Tanzania kwenye upande wa Mbuga za Wanyama ambapo alikuja Ngorongoro na Mpenzi wake mwaka 2017.

 

 

Exit mobile version