Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Morocco zinaeleza kuwa klabu ya FAR Rabat ya nchini humo imetuma ofa kwenda klabu ya Simba kwaajili ya kuihitaji saini ya kocha wa klabu ya Simba Fadlu Davies.
FAR Rabat imemtimua kocha wake Hubert Velud na wanahitaji kocha mwingine ambaye ataiongoza klabu hiyo kufikia malengo yao na Fadlu ndiye lengo lao kubwa kwa sasa.
Hata hivyo klabu hiyo itakua na kazi kubwa ya kufanya ili kumnasa kocha huyo kutokana na kuwa na mkataba na klabu hiyo aliyojiunga nayo msimu huu.
Pia pamoja na hilo FAR Rabat watapata wakati mgumu kutokana na kocha huyo kuwa na project ndefu na klabu hiyo ya kuirudisha katika makali yake baada ya kukosa ubingwa kwa takribani misimu mitatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Fadlu amefanikiwa kuirudisha Simba Sc katika makali yake ambapo kwanza imekua na soka la kuvutia huku ikipata alama katika michezo ya ndani na nje ya nchi kiasi cha kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

