Kocha wa Simba Sc Fadlu Davids ametozwa faini ya sh 2,000,000 kwa kutoa shutuma dhidi ya bodi ya ligi akidai kuwa wana ajenda tofauti dhidi ya timu yake kuhusiana na ratiba ya michezo ya ligi kuu ya klabu hiyo.
Kocha huyo alizungumza hayo mbele ya wadhamini wenye haki ya matangazo Azam TV baada ya mchezo dhidi ya Singida Black stars wakati akifanyiwa mahojiano ya baada ya mchezo kituo hicho kaka ulivyo utaratibu wa kikanuni.
Fadlu alikaririwa akisema kuwa bodi ya ligi imewapangia ratiba ngumu Simba Sc bila kujali muda na afya za wachezaji.
“Bodi ya ligi hawajatutendea haki kutuchezesha kila baada ya masaa 48 kinyume na utaratibu wa kujali afya za wachezaji na hili sio sawa hata kidogo”,Alisema Fadlu.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni 45:2(2.9) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa makocha.