Imefahamika kuwa klabu ya Simba Sc itacheza mchezo wake wa marudiano wa Fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Fainali hizo zitachezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itachezwa nchini Morocco Mei 17 2025 na marudiano kufanyika nchini Mei 25 2025.
Simba sc imefanikiwa kufuzu fainali hizo baada ya kuifunga Stelleboch Fc kwa matokeo ya jumla ya 1-0 baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa marudiano nchini Afrika ya kusini huku mchezo wa kwanza Visiwani Zanzibar Simba sc iliibuka na ushindi wa 1-0.
Mchezo wa pili wa fainali huwa na faida kwa klabu mwenyeji kutokana na mchezo huo kuwa ndio maalumu wa kukabidhi kombe na huwa na msisimko mkubwa wa mashabiki wa nyumbani.
Simba sc inapewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe hilo ambalo halijawahi kuchukuliwa na klabu yeyote hapa nchini Tanzania.