Home Soka Farid Mussa Asalia Yanga sc

Farid Mussa Asalia Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Farid Mussa wa Yanga sc amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kusalia klabuni hapo baada ya ule wa awali kumaliziki Juni 30 mwaka huu ambapo usajili huo ni pendekezo la kocha Miguel Gamond kusalia na nyota huyo kwa ajili ya msimu ujao.

Farid pamoja na kusaini mkataba wa kusalia Yanga sc bado ana kazi kubwa ya kufanya kumshawishi Gamond amuanzishe mara kwa mara kikosini humo kutokana na uwepo wa mastaa wakubwa kama Pacome Zuozuo,Stephane Aziz Ki na ongezeko la Cletous Chama.

Tangu ajiunge na Yanga sc msimu wa 2020 kiungo huyo amefanikiwa kuchukua makombe makubwa yote ya ndani kwa misimu mitatu mfululizo huku misimu miwili ya 2023/2023 na 2023/2024 akisota kupata namba katika kikosi cha kwanza mara kwa mara.

banner

Yanga sc imeamua kusalia na asilimia kubwa ya nyota wake wazawa kutokana na ukweli kwamba wachezaji hao ni wazoefu na wana viwango vikubwa isipokua wanazidiwa uwezo na mastaa wa kigeni walio na ubora mkubwa zaidi hivyo kuwaacha ni ngumu kupata mbadala kwa wachezaji wa ndani kirahisi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited