Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes ametupilia mbali ofa nono kutoka Al Hilal ya Saudi Arabia kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo ya ligi kuu ya Saudi Pro huku akitaka kuendelea kusakata kabumbu barani Ulaya.
Bruno (30) raia wa Ureno amefanya maamuzi ya kukataa ofa nono ya mshahara wa pauni laki 7 kwa wiki (takribani Tsh bilioni 2.55) huku akichagua kusalia Manchester United, timu iliyomaliza nafasi ya 15 msimu uliomalizika huku ikipoteza mchezo wa fainali ya Europa League.
Staa huyo anataka kubaki barani ulaya hata kama haitokua katika klabu yake ya Manchester United ambayo iko tayari kumuachia ili kupunguza matumizi klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo staa huyo bado anazitamanisha klabu za Real Madrid pamoja na Bayern Munich ambazo zinamuangalia kwa karibu kama moja ya suluhisho la muda mfupi katika maeneo ya viungo katika klabu hizo.