Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) linatarajia Kufanya uchunguzi wa mpira wa Tanzania katika Kipindi cha miezi miwili nyuma hadi sasa kutokana na migogoro ya kimaamuzi iliyotokea.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa kamati ya nidhamu FIFA ilituma barua kwenda TFF mnamo Juni 13, 2025 ikiwataarifu kuwa inafuatilia mienendo ya soka la Tanzania ikiwa ni pamoja viashiria vya siasa kuingilia masuala ya soka.
Aidha FIFA imeitaka TFF kutoa ushirikiano katika uchunguzi wao huo hatua inayokuja kufuatia sintofahamu iliyotokea kwenye soka la Tanzania kwa kipindi cha miezi mitatu tangu kuahirishwa kwa Derby ya Kariakoo mnamo Machi 8.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pamoja na Taarifa hiyo pia FIFA imeitaka TFF kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wa FIFA watakaokuwepo nchini kwa ajili ya ukaguzi huo ambapo pia watakagua masuala ya fedha na maamuzi.