Site icon Sports Leo

Flamengo Waizima Chelsea Kibabe

Klabu ya Flamengo Fc ya nchini Brazil imefanikiwa kuifunga klabu ya Chelsea kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kundi D uliofanyika jana usiku Philadelphia nchini Marekani.

Chelsea ilipata bao la mapema la Pedro Neto dakika ya 13 katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Lincoln nchini humo ambapo bao hilo lilisawazishwa na Bruno Henrique dakika ya 62 huku mshambuliaji mkongwe Danilo alifunga bao la pili kwa flamengo dakika ya 65 ya mchezo.

Ugumu ulizidi kwa Chelsea baada ya Nicholas Jackson kutolewa kwa kadi nyekundu dakika chache baada ya kuingia uwanjani huku Wallace Yan akiweka uhakika wa alama tatu kwa Flamengo Fc alipofunga bao la tatu dakika ya 83.

Sasa Chelsea wanapaswa kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Es Tunis ili kufuzu hatua inayofuatia ya robo fainali.

Exit mobile version