Site icon Sports Leo

Fomu Kumrithi Karia Laki 5

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) inatangaza tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika tarehe 16/08/2025 jijini Tanga.

Kamati hiyo imetangaza kuwa nafasi zinazogombewa ni nafasi ya Rais wa shirikisho hilo (Nafasi 1) na nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji (Nafasi 6) ambao ndio wanatimiza safu ya uongozi wa shirikisho hilo la soka nchini

Gharama za kuchukua fomu kwa nafasi ya Rais ni Tsh 500,000 na Shilingi 200,000 kwa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambapo wote wenye vigezo wamekaribishwa kuchukua fomu hizo.

Tayari Rais wa sasa wa Shirikisho hilo ameahidi kuchukua fomu kuendelea na nafasi hiyo huku staa wa zamani ya Yanga sc Ally Mayai naye akipigiwa upatu kuchukua fomu kupambana na karia.

Fomu zitaanza kutolewa kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 16 hadi 20/06/2025 saa 10 kamili jioni. Fomu zinapatikana Makao Maku ya TFF na kwenye tovuti ya TFF.

 

 

Exit mobile version