Home Soka Gamondi Anukia Apr ya Rwanda

Gamondi Anukia Apr ya Rwanda

by Sports Leo
0 comments

Kwa mujibu wa taarifa nyingi kutoka Kigali nchini Rwanda inaelezwa aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi upo uwezekano akajiunga na APR ya Rwanda ambapo mazungumzo yameanza ili kukamilisha dili hilo.

Katika mazungumzo ambayo kwasasa yapo katika hatua za awali kuona kama kuna uwezekano wa Miguel Gamondi kujiunga hiyo inayomilikiwa na Jeshi la ulinzi la nchi hiyo huku utata mkubwa ukiwa katika mshahara na stahiki zingine za kimkataba za bosi huyo.

Ikumbukwe Gamondi aliachana na Yanga sc wiki iliyopita kwa makubaliano ya pande mbili baada ya mabosi wa klabu hiyo kutoridhishwa na mwenendo mbaya wa kikosi hicho huku pia vipigo dhidi ya Azam Fc na Tabora United vikichagiza mwisho wa kocha huyo.

banner

Endapo itafanikiwa kumsajili kocha huyo Apr itafaidika na uzoefu wake na aina yake ya ufundishaji ambapo ni muumini wa soka la kasi lenye pasi nyingi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited