Site icon Sports Leo

Ghana Watolewa Afcon 2022

Kinyume na matarajio ya wadau wengi wa soka barani Afrika,Timu ya taifa ya Ghana ‘black Stars’imetupwa nje ya michuano ya Afcon 2022 inayoendelea nchini Cmaeroon baada ya kukubali kichapo cha 3-2 kutoka kwa Comoro mchezo uliofanyika katika uwanja wa Roumdé Adjia Stadium nchini humo.

Comoro wanaoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza walianza kupata bao la uongozi mapema dakika ya nne Elfadou Mohamed ben Nabouhane huku staa Ahmed Mogne akiongeza bao la pili dakika ya 61 kipindi ambacho Ghana wakiwa pungufu baada ya Andrew Ayew kupewa kadi nyekundu kufuatia kumchezea madhambi golikipa wa Comoro.

Ghana walicharuka na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 64 kupitia kwa Richmond Boakye huku pia dakika 13 baadae walisawazisha kupitia kwa Alexander Djiku na kufanya ubao usomeke 2-2 lakini dakika 5 kabla ya kipenga cha mwisho Comoro walipata bao kupitia kwa Ahmed Mogni ambaye alifunga mabao 2 na kuwafanya Ghana kuyaaga mashindano tofauti na matarajio ya wadau wengi.

Kutokana na matokeo hayo sasa rasmi Moroco na Gabon ndio wanafuzu kupitia kundi C huku Ghana akiyaaga mashindano hayo na Comoro akisikilizia kama atapata nafasi ya kuendela kama ‘best Looser’.

Exit mobile version