Sports Leo

Himid Mao Atua Azam Fc

Sasa rasmi kiungo Himid Mao Atua Azam Fc kwa mkataba wa miaka mmoja akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Ghazl El Mahalla ya Misri aliyokua akiitumikia.

Kiungo ametambulishwa rasmi na uongozi wa Azam fc kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo sass anaungana na Aishi Manula na Ahmed Pipino pamoja na makinda wawili wapya ambao ndio usajili uliokamilika mpaka sasa Azam Fc.

Himid Mao alitokea katika klabu hiyo na kuamua kucheza soka la kimataifa nchini Misri kwa takribani miaka mitano na sasa anarejea Azam Fc sehemu ambapo alikulia kuanzia katika levo ya akademi ya timu hiyo.

Kiungo huyo wa ukabaji alianza soka mwaka 2005 kisha akaingia akademi ya Azam Fc mwaka 2007 kisha mwaka 2009 akajiunga timu kubwa na msimu wa 2013-2014 aliisaidia Azam Fc kushinda ubingwa wa ligi kuu akifunga bao muhimu dhidi ya Ruvu Shooting kisha baada ya miaka 11 aliondoka klabuni hapo na kujiunga na Petrojet ya Misri.

 

 

Exit mobile version