Sports Leo

Ibenge Amsajili Kanoute Azam Fc

Kocha wa klabu ya Azam Fc Frolent Ibenge amependekeza usajili wa kiungo Sadio Kanoute ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuwa huru kutokana na kumaliza mkataba na klabu ya Js Kabylie ya nchini Algeria aliyojiunga nayo akitokea Simba Sc.

Ibenge amevutiwa na uzoefu wa mazingira ya hapa nchini ambapo kiungo huyo alishakaa na hivyo hatosumbuka kuzoea kitu ambacho kinampa faida ya kuwa na utulivu uwanjani moja kwa moja huku pia uwezo wake wa kucheza kama kiungo wa kuzuia au kushambulia ukiwa na faida zaidi kwa timu hiyo.

Ibenge Amsajili Kanoute Azam Fc-sportsleo.co.tz

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Simba sc amejiunga na Azam Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo akionyesha uwezo mkubwa basi anaweza kuongezewa zaidi kuendelea kusalia klabuni hapo.

Msimu huu Azam Fc imeonyesha dalili njema za kufanya vizuri kutokana na kusajili mwalimu mzoefu wa ligi kubwa barani Afrika Frolent Ibenge ambaye pia moja ya wasaidizi wake Annicet Kiazayidi ana uzoefu wa kutosha wa ligi kuu hapa nchini baada ya kuifndisha Tabora United msimu uliopita ambapo timu hiyo ilikua tishio zaidi.

Ibenge pia amefanya usajili wa mastaa wa kutosha kikosini humo ambapo amewasajili wachezaji wazoefu kama Himid Mao Mkami,Edward Charles Manyama,Jephte Kitambala,Pape Doudou Diallo,Aishi Manula na beki Lameck Lawi ambao moja kwa moja wataongeza uzoefu kikosini humo.

Moja ya kazi kubwa ya kwanza ya Ibenge ni kuhakikisha kuwa klabu hiyo inafanya vizuri katika ligi kuu ya ndani na nje ya nchi hasa katika michuano ya kimataifa ambapo haijawahi kuvuka hatua ya makundi hata mara moja katika historia ya klabu hiyo.

Katika michuano ya kimataifa msimu huu Azam Fc itaanzia hatua ya awali ya kombe la shirikisho ambapo itavaana na Al Merrekh ya Sudan mwezi septemba mwaka huu.

Exit mobile version