Home Makala Ibenge Kutua Azam Fc

Ibenge Kutua Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc ipo katika hatua za mwisho kumalizana na kocha Frolent Ibenge kuchukua nafasi ya Rachid Taoussi kuifundisha klabu hiyo yenye makazi yake Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mabosi wa klabu hiyo hawana mpango wa kuendelea na kocha Taoussi pamoja na benchi lake la ufundi hivyo wameamua kutafuta kocha mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Ibenge ameonekana ni chaguo sahihi kwa mabosi hao na sasa wanapambana kumalizana nae hasa upande wa mshahara ambao umeonekana kuwa kikwazo kikubwa ambapo analipwa zaidi ya milioni 150 na klabu yake ya sasa ya Al Hilal Fc.

banner

Al Hilal Fc na Ibenge nao ndoa yao inaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu ambapo sasa Azam Fc wanaona wana kazi rahisi ya kumshawishi jambo ambalo linaelekea kutimia.

Inaarifiwa kuwa Ibenge ameridhika na projekti ya Azam Fc baada ya kufika nchini siku ya Jumamosi na kutembelea klabu hiyo akiridhishwa na miundombinu ya klabu hiyo na sasa kikwazo pekee kimebaki ni makubaliano ya mshahara pekee.

Hata hivyo ni kama suala hilo linaweza kukamilika muda wowote kutokana na mabosi wa Azam Fc kuwa sio wabahili katika kutoa mishahara mikubwa kwa mastaa wanaowahitaji.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited