Klabu ya Simba sc imetangaza kuanza kuuza jezi za klabu hiyo za msimu mpya wa 2021/2022 kuanzia leo huku uzinduzi rasmi wa jezi hizo ukifanyika mapema kesho baada ya jezi hizo kuvuja.
Awali ilitangazwa mapema kwamba jezi hizo zingeanza kuuzwa siku ya jumamosi mapema baada ya uzinduzi lakini kuvuja kwa jezi hizo kumeifanya klabu hiyo kuchukua maamuzi ya kuanza kuziuza mapema hii leo.
“Watu hawapendi mafanikio yetu ndio maana wamevujisha jezi zetu,Kuna timu kama Coastal union wametoa jezi lakini hazikuvuja, imefika Simba jezi zimevuja hii ni tabia mbaya”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Kwa nini uvujishe jezi ya timu ? Tukianza utani wa jadi wa kuvujisha jezi tunapokwenda itakuwa ni vita”Alisema Msemaji wa mklabu hiyo Ezekiel Kamwaga wakati akiongea na waandishi wa habari mapema hivi leo.
Klabu ya Simba sc iliingia makubaliano na kampuni ya Vunjabei Group kuhusu kusambaza jezi za klabu hiyo kwa gharama ya shilingi bilioni mbili kwa misimu miwili kusambaza jezi za klabu hiyo