Site icon Sports Leo

Jkt Tanzania Walipa Kisasi Simba

JKT Tanzania wamelipa leo kisasi dhidi ya Simba Sc kwa kuwachapa bao 1-0 katika michuano ya ligi kuu bara katika uwanja wa Uhuru ambapo mchezo wao wa kwanza walipokutana na Simba walifungwa mabao 3-1.

Bao pekee la ushindi limefungwa kupitia Adam Adam dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza cha mchezo ambalo limedumu mpaka mwisho wa kipindi.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo la kisasi pia nyota wapya wa Simba Luis na Shiza Kichuya wameanza leo kwa mara ya kwanza.

Exit mobile version