Uongozi wa Kaizer Chiefs utajaribu kutimiza ndoto za mashabiki wao kwa kumpata Feisal Salum kutoka klabu ya Azam Fc licha kuwa mchezaji huyo ana ofa nyingi ndani na nje ya nchi.
Mashabiki wa Kaizer Chiefs wanaamini Feisal ni mchezaji sahihi kwao ambaye anaweza kuirudisha timu yao katika hadhi ya kimataifa, Kaizer wanataka kutengeneza timu kupitia yeye.
Hata hivyo usajili huo unatemea na uwepo wa kocha Nasredine Nabi ambaye mpaka sasa amekalia kuti kavu klabuni hapo licha ya kuipatia klabu hiyo taji la kwanza baada ya miaka kumi kupita.
Feisal ana machaguo mengi sana sababu ofa mezani kwake ziko za kutosha lakini Kaizer Chiefs wanaonesha nia ya dhati kweli huku mchezaji mwenyewe akionekana kuvutiwa na dili hilo.
Inasemekana Nabi anawasiliana na Feisal moja kwa moja na mchezaji amekubali kujiunga na Kaizer kutokana na heshima yake kwa kocha huyo aliyembadilisha nafasi kutoka kiungo wa chini kuwa kiungo mshambuliaji jambo ambalo limempandisha thamani yake mpaka sasa.