Klabu ya Azam Fc itaondoka nchini Tanzania na wachezaji 14 Kuelekea Nchini Morocco kwa ajili ya Maandalizi ya Msimu Ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa (pre-season) hasa baada ya kupata uhakika wa kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Mastaa wa Azam Fc watajiunga na kambi mwanzoni mwa mwezi Julai kisha wataweka kambi ya muda mfupi wa wiki moja Zanzibar kisha kusafiri kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kambi hiyo huku wachezaji wengine watajiunga na timu moja kwa moja nchini humo.
Tayari kikosi hicho kinaendelea kufanyiwa maboresho kukidhi mahitaji ya benchi la ufundi chini ya kocha Yousouph Dabo ambapo mastaa kama Daniel Amoah,Charles Edward na Ayoub Lyanga wameachwa kikosini humo huku Adam Adam,Ever Meza na mshambuliaji jhonier blanco wakiwa wamesajiliwa kujiunga na kikosi hicho mpaka sasa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.