Kengold Fc Kuungaunga Mpaka Tabora

by Dennis Msotwa
0 comments

Wachezaji wa timu ya KenGold FC kila mmoja anasafiri kivyake kwenda mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini dhidi ya Simba Sc utakaofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Juni 18 2025.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu ni kuwa imeamuliwa wachezaji wa timu hiyo ya wakubwa ambao walikua wametawanyika sasa wanakutana Tabora ambapo kila mchezaji katumiwa nauli asafiri kivyake mpaka mkoani humo.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya vijana KenGold FC na viongozi wameondoka tayari  kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo huo.

Awali timu hiyo ilituma ombi lao la kucheza Dar Es Salaam katika uwanja wa KMC Complex ambalo lilikataliwa na Bodi ya ligi nchini kwa madai limetumwa nje ya muda wa kikakuni.

banner

Tayari klabu hiyo imeshuka daraja na sasa inafanya kukamilisha ratiba ili isipate adhabu ya kufunguwa na shirikisho la soka nchini.

You may also like

Leave a Comment

Enable Notifications OK No thanks