Mchezo wa ligi kuu ya Nbc Kati ya klabu ya KMC Fc dhidi ya Simba Sc Umebadilishwa na sasa Utachezwa katika uwanja wa Kmc Complex jijini Dar Es Salaam Mei 11 ambayo ni siku ya Jumapili, saa kumi jioni.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora ambapo Kmc kama wenyeji wa mchezo walitumia haki yao ya kikanuni kuuhamishia mchezo huo mkoani humo kwa lengo la kupata mapato zaidi.
Hata hivyo chanzo kikuu cha mchezo huo kurudishwa jijini Dar es Salaam ni kutokana na mazungumzo baina ya klabu hizo mbili ili kuipa nafasi muhimu zaidi klabu hiyo kujiandaa na mchezo wa kwanza wa fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane nchini Morocco Mei 17 2025.
“Sisi tulitumia kanuni kutaka kuhamisha mchezo kwa sababu zetu za msingi lakini baada ya Simba kutinga fainali, Menejimenti ya juu ya Kmc na ya Simba Sc zilikubaliana kuwa mchezo wao upigwe Dar es Salaam na sio Tabora tena ili tuwape nafasi wenzetu Simba kuendelea kujiandaa zaidi na safari na vitu vingine”,Alisema Khalid Chukuchuku, Afisa habari wa Kmc Fc.
Tayari pande zote mbili zimeshapewa taarifa hizp rasmi pamoja na Mamlaka za mpira nchini kuhusu uamuzi huo.