Home Soka Kocha Msaidizi Atua Yanga Sc

Kocha Msaidizi Atua Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha Mustafa Kodro kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Mussa Ndaw ambaye ameondolewa sambamba na Kocha Miguel Gamondi kupisha mabadiliko mapya klabuni hapo.

Mustafa ni pendekezo la kocha mkuu Sead Ramovic ambaye wamefanya kazi pamoja katika klabu ya Ts Galaxy inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya Kusini.

Kocha huyo baada ya kutambulishwa moja kwa moja aliwasili kambini kwa klabu hiyo iliyopo Kigamboni Avic Town na kuanza moja kwa moja kuwanoa mastaa wa timu hiyo waliopo kambini licha ya baadhi ya mastaa kuwa katika majukumu ya timu za Taifa.

banner

Sead na Mustafa wamefanya kazi wote katika klabu ya Ts Galaxy ambapo walitengeneza timu imara inayocheza mchezo mzuri ikijenga mashambulizi kuanzia nyuma huku ikifanikiwa kuwavimbia vigogo Mamelod Sundowns,Kaizer Chiefs na Orlando Pirates katika michezo mbalimbali ya ligi kuu na michuano mingine nchini humo kabla ya mabosi wa klabu hiyo kuamua kuuza mastaa wake wakubwa wakati wa dirisha dogo la usajili mwaka huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited