Home Makala Kramo Hatarini Simba sc

Kramo Hatarini Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Pamoja na kwamba amesajili msimu huu klabu ya Simba inapanga kuachana na winga Aubin Kramo hasa kwenye dirisha dogo la mwezi Januari kufuatia majeraha yaliyomuandama na kumuweka nje kwa muda mrefu.

Winga huyo raia wa Ivory Coast hajacheza mchezo wowote rasmi klabu hapo tangu asajiliwe msimu huu kutokea klabu ya Asec Mimosa ya nchini kwao ambapo kwa  sasa yuko nchini kwao kwa ajili ya matibabu baada ya kuumia katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Mo Simba Arena.

Hatua hiyo inafuatia nia ya viongozi wa Simba kutafuta nafasi ya kumsajili mchezaji mwingine atakayeziba pengo la Kramo kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo klabu hiyo imefuzu hatua ya makundi huku ikiweka lengo la kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited