Licha ya kukosa wachezaji sita ambao walikutwa na Virusi vya Corona bado Manchester City imeweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea na kuzidi kuweka rehani nafasi ya Frank Lampard kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Mpaka dakika ya 16 mabao ya Ikay Gundogan,Phil Foden na Kevin De Bryune yalitosha kuipa Man cityb uongozi wa mchezo ambapo Chelsea walipata bao la kufutia machozi dakika mbili za nyongeza ya mchezo.
Man city imepaa mpaka nafasi ya tano ya msimamo na alama 29 nne nyuma ya Man United na Liverpool huku Chelsea ikisalia na alama 26 katika nafasi ya nane ya msimamo.