Home Soka Lawi Aaga Coastal Union

Lawi Aaga Coastal Union

by Sports Leo
0 comments

Mlinzi wa kati wa klabu ya Coastal Union ya Jijini Tanga Lameck Lawi amewaaga wapenzi na Mashabiki wa klabu hiyo baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Kmc kutamatika na kuisaidia timu yake kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mlinzi huyo inasemekana tayari ameshamalizana na klabu ya Simba sc ambayo atajiunga nayo hivi karibuni baada ya kufikia makubaliano baina ya vilabu hivyo na makubaliano binafsi ya mchezaji huyo.

Taarifa za ndani ya uongozi wa klabu ya Coastal Union zimethibitisha kuwa vilabu vya Coastal Union na Simba vilikwisha kamilisha kila kitu kwa maana ya makubaliano ya ada ya usajili ya mlinzi na makubaliano mengine muhimu ya kimkataba.

banner

Lawi anatajwa kwenda kuungana na Che Fondoh Malone kwa ajili ya kutengeneza ukuta muhimu klabuni hapo kwa ajili ya msimu ujao ambapo inaonekana Henock Inonga hatokuwepo baada ya kupata ofa nono nje ya Tanzania huku Coastal Union ikimchukua beki Hussein Kazi katika sehemu ya makubaliano ya usajili huo.

Coastal Union kwa msimu ujao itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho ambapo inalazimika kupanga vizuri kikosi chake kwa ajili ya michuano hiyo ambapo italazimika kuwabakisha baadhi ya nyota wake kikosini mwake.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited