Mkataba wa kiungo wa Newcastle United ,Matty Longstaff unameguka Juni 30 msimu huu, huku Klabu ya Ac Milan ikiwa kwenye mstari wa mbele kuisaka saini yake.
Longstaff yupo tayari kuongeza kandarasi nyingine iwapo klabu hiyo itakamilisha dili la kupata mmiliki mpya wa klabu hiyo.
Nyota huyo mwenye miaka 20 imeelezwa kuwa yupo tayari kufanya kazi na bosi mpya anayetajwa kuwa mmoja ya wamiliki wa klabu hiyo ambayo ni kampuni kutoka Uarabuni.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msimu huu Longstaff amecheza mechi 13 ambapo alianza kwenye mechi 11 amefunga mabao matatu kwenye jumla ya mashindano yote.